Kapombe aliifungia Azam bao la kwanza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga lililoipa nguvu timu yake na hatimaye John Bocco kusawazisha kisha Kapombe akafunga moja ya penati nne zilizoipa Azam ubingwa mbele ya Yanga.
“Ni mechi yangu kubwa ya kwanza tangu nimerejea uwanjani baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda na nashukuru niliweza kufunga goli, goli hilo lilikuwa zawadi kwa mashabiki wote waliokuwa wakiniombea pamoja na familia yangu kwa ujumla,” alisema Kapombe baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Azam iliifunga Yanga kwa penati 4-1 na kuchukua Ngao hiyo.
“Timu yetu iko vizuri, kila siku mwalimu anaendelea kuiandaa ili kila wachezaji kuzoena kwasababu sasahivi kuna sura nyingi mpya lakini mwalimu anafanyia kazi hilo kwa ajili ya msimu wa ligi.”
“Nitajitahidi kufanya mazoezi ili niridi katika kiwango changu kama msimu uliopita, mashabiki waendelee kuwa pamoja na mimi na kuni-support.”
Kapombe anaamini kutakuwa na ushindani mkubwa kwenye ligi msimu huu kutokana na aina ya usajili uliofanywa na timu huku kila timu ikiwa imejiandaa kufanya vizuri kwe ligi kuu Tanzania bara.
“Ushindani utakuwa mkubwa zaidi ya msimu uliopita kwasababu kila timu ambayo ipo kwenye ligi pamoja na zile zilizopanda zote zimefanya usajili vizuri kwa ajili ya kufanya vizuri msimu huu lakini bado Azam naipa nafasi ya kwanza.”
0 comments:
Post a Comment